ID 9445E7
Nina umri wa miaka 39 na nimekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka miwili hivi. Kitu pekee nilichofanya ni kumpenda mke wangu kwa dhati. Nilimpenda zaidi alipobeba ujauzito. Lakini nilishtuka na kuvunjika moyo sana nilipoona mtoto wetu ana ngozi ya rangi ya nyeupe badala ya nyeusi.
Kwa kuwa mimi na mke wangu wote ni weusi, bado sikuweza kuelewa mtoto mweupe alitokeaje. Mtoto hafanani na mimi kabisa, japokuwa anafanana sana na mama yake. Kwa zaidi ya miezi sita, licha ya maumivu makali moyoni mwangu, niliamua kukaa kimya. Sikusema wala kuchukua hatua yoyote. Nilifanya hivyo kwa sababu nilitaka kuwa na uhakika kabisa na kutompa mke wangu faida ya shaka, nikitumaini labda rangi ya mtoto ingebadilika.
Najua watoto wengi huzaliwa weupe lakini hupata rangi yao halisi baada ya miezi kadhaa. Nilisubiri miezi sita, kisha nikaongeza miezi mingine sita, nikiomba tu hofu yangu iwe ya uongo. Lakini hakuna kilichobadilika. Sasa ni zaidi ya mwaka mmoja, na rangi bado ni ile ile.
Nimevunjika moyo sana. Nilikuwa na imani kubwa na upendo wa dhati kwa mwanamke huyu, lakini alinisaliti. Alifanya mapenzi na mwanaume mwingine, akabeba mimba yake, kisha akajaribu kunipandikizia mtoto huyo kama ni wangu. Mama yangu alinashauri nisimwoe, lakini nilipuuza ushauri wake. Yani nilimuoa ndo aje kuniaibisha namna hii!!.
Kwa zaidi ya miezi sita sasa, sijamgusa mke wangu, sili chakula chake, wala simkaribii mtoto. Nilifanya hivyo kama ujumbe wazi, nikimpa nafasi ya kusema ukweli na kuomba msamaha. Lakini bado anajifanya hana hatia, analia karibu kila siku na kuniuliza, ‘Nimekufanyia nini?’ kana kwamba hajui chochote.
Ukweli ni kwamba siwezi kuvumilia wazo la kupoteza muda na fedha zangu nikilea mtoto wa mwanaume mwingine. Ili kupunguza maumivu yangu, nilianza kuonana na mwanamke mwingine. Tumekuwa pamoja kwa zaidi ya miezi sita sasa.
Ni mwanamke mzuri sana, na nimependa kwa dhati. Kwa kweli, kwa sasa ana mimba yangu. Nilimwambia mama yangu kuhusu yeye, naye alisisitiza nimuoe mara moja. Tukakusanya wajomba wachache na kukamilisha ndoa ya kimila wiki iliyopita.
Mke wangu wa kwanza hajui chochote kuhusu mwanamke huyu mwingine, kwa sababu sijawahi kumwambia. Kwa uaminifu kabisa, mapenzi yangu kwake yamekufa kabisa. Kumuona yeye na mtoto wake kunaniumiza na kunikera sana. Ninampenda sana huyu mwanamke mpya na sitaki kumpoteza.
Hali hii ni ngumu kidogo kuisimamia.
Comments
No comments yet. Be the first to share a thought.