ID A654AF
Nilimwoa mume wangu kwa upendo mkubwa sana, nikiwa na uhakika kuwa ndoa ni ushirikiano wa kweli. Nilipata mimba, tukafurahi wote. Lakini baada ya kujifungua, kila kitu kilibadilika. Alianza kunitazama kama mzigo. Aliniambia mtoto hafanani na yeye.
Maneno hayo yaliumiza zaidi kuliko uchungu wa kujifungua. Nilikaa kimya nikijua ukweli upo, lakini moyo wangu ulianza kufa polepole. Nilienda hadi kwa wachungaji kuhusu hili swala la mume wangu kuacha kutujali, lakini sikufanikiwa, nilijaribu hadi kushirikisha ndugu zake lakini sikufua dafu maana walisema hawaoni shida yoyote na ubaya yule mwanaume akiitwa kujielezea kama ameisusa familia, anakataa kabisa.
Hali ile iliniendelea kunitafuna kadri ya siku zinavyoenda, nikiangalia tuna nyumba na mtoto ni wake sababu sijawahi kumsaliti nikiwa kwenye ndoa yetu na mimba ilikua ya kwake na mtoto ni wa kwake ila simuelewi asemavyo mtoto hafanani nae wakati anaonekana kabisa ni wa koo yao.
Ni muda umepita hata majukumu yake kama mume hayatimizi tukiwa chumbani, mwanzoni nilihisi labda amechezewa akili, lakini haikua hivyo maana nimeomba kila aina ya maombi bila mafanikio.
Uzuri hata kama anasema mtoto si wake lakini mahitaji mengine anamfanyia mfano ada za shule , chakula lakini ule ukaribu ndo unaokosekana, lakini niliamua kumuachia mungu, na ubaya na mimi nikajikuta nimeingia kwenye mambo ya kidunia.
Leo hii ninaishi naye tu sababu ya mtoto, lakini haja zangu zingine nazitimiza nje ya ndoa na wala hajali kuhusu hilo. ndoa hizi zina mswahibu sana jamani, msione watu wanacheka mbele yenu, yaliyomo ndani ni kama tanuri la moto.
Comments
No comments yet. Be the first to share a thought.